Kauli ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba ya kutaka Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kuelekeza dola 1.3 bilioni za Asasi za Kiraia kwenda kwenye miradi ya kipaumbele ya Serikali ya Awamu ya Sita, imekosolewa na wadau wa asasi hizo.
Akiandika katika ukurasa wake wa Twitter, Dk Mwigulu amesema walikuwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Emmanuel Tutuba katika mkutano na Mkurugenzi wa Shirika hilo, Kate Somvongsiri.
“Nimeiomba @USAID kuelekeza msaada wa Dola Bilioni 1.3 sawa na zaidi ya Shilingi Trilioni 3 inazotaka kuipatia Tanzania kupitia Asasi za Kiraia, zielekezwe kwenye miradi ya kipaumbele ya Serikali ya Awamu ya Sita. Tutazisimamia vizuri,” ameandika Waziri Mwigulu.
Akichangia katika Twitter hiyo, Okumu Kembo Migire amehoji: “Seriously? Mnajua CSOs, FBOs na NGOs ngapi zimeajiri Watanzania na wanategemea miradi hiyo?
Naye Anderson Ndambo amesema kuwa kuzitaka fedha hizo kunalenga kuondoa uwezo wa Azaki kusaidia jamii hasa katika eneo la haki za binadamu.
“Kuondoa ukosoaji dhidi ya Serikali kwa kuziminya Asasi za Kiraia.”
Kwa upande wake Hancy Machemba