Zungu ashauri kujengwa kituo cha Polisi Daraja Tanzanite

Naibu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu ameshauri kujengwa kituo cha Polisi jirani na Daraja la Tanzanite ili kuimarisha ulinzi wa kulinda madhari ya mradi huo uliojengwa kwa fedha nyingi.

Hayo ameyasema leo Machi Machi 24, 2022 katika uzinduzi wa mradi wa daraja la Tanzanite jijini Dar es Salaam, lililogharimu Sh243 bilioni.

Zungu ambaye ni Mbunge wa Ilala amesema kuna tabia ya watu wasiokuwa waaminifu wenye tabia ya kufungua vyuma na kwenda kuuza mitaa huku akimuomba Mkurugenzi wa Jiji hilo na Meya kusimamia mradi huo kwa kushirikiana na mwekezaji.

“Tunaona uchafu umeanza kutupwa kwenye daraja hili na jua leo wamesafisha ni wasihi wananchi watanzania turudishe heshima yetu daraja lisafishwe vijana muache kuchora mambo ya ajabu ajabu,

 “Ulinzi uimarishwe na kujengwe kituo cha Polisi ili kuimarisha ulinzi wa daraja hili lilojengwa kwa gharama kubwa pamoja na miundombinu yake kwa sababu kunatabia ya watu kuja kufungua vyuma na kwenda kuuza mtaani nawaomba Mkurugenzi na Meya msaidiane na muwekezaji,”amesema Zungu

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii