RAISI SAMIA ATOA NENO KWA WALIOKUA WAKISEMA MIRADI YA HAYATI MAGUFULI HAITIENDELEZWA

Rais Samia Suluhu Hassan amesema watu waliokuwa wakisema miradi iliyaochwa na mtangulizi wake, Hayati John Magufuli haitaendelezwa, hawakuwa sahihi kwa sababu Serikali inayoongoza nchi ni ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Rais Samia ameeleza hayo leo Jumatano Machi 23, 2022 wakati akizindua nyumba hizo, zilizojengwa kwa thamani ya zaidi ya Sh51 bilioni na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), mchakato wa ujenzi huo ulianza 2016.

 “Kulikuwa na maneno mengi, iliyoachwa haitaendelezwa ukiuliza sababu hakuna. Hakukuwa na sababu ya kwamba miradi hiyo isiendelezwe, kwani ilianzishwa na kuagizwa ndani ya Ilani ya CCM. Sasa kwa kunitazama sura na kusema isingeweza kutekelezeka miradi nadhani hekima haikutumika.

“Wanaposema miradi haitaendelezwa nadhani upeo wao wa kufikiria ni mdogo sana. Hata miradi hii ilivyoanzishwa nilikuwa Makamu wa Rais, kwa hiyo ni sehemu tangu kuanza kwake na kutekelezwa,” amesema Rais Samia wakati akizindua mradi wa nyumba 644 za Magomeni Kota. 

Hata hivyo, Rais Samia akiwahutubia wakazi wa Magomeni na wananchi mbalimbali wa mkoa wa Dar es Salaam amesema “lakini tuwaombe nasi tujiombee kwa Mungu atupe nguvu, uwezo  na hekima zaidi ili tuweze kuendeleza miradi kwa maendeleo ya Taifa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii