Dunia yaomboleza mwanadiplomasia mahiri wa Marekani Madeleine Albright

Washington,Wanadiplomasia na viongozi mbalimbali duniani kote wanaendelea kutuma risala za rambi rambi kwa familia ya Madeleine Albright, mwanamke wa kwanza waziri wa mambo ya nje wa Marekani na mmoja kati ya wanawake wenye ushawishi mkubwa, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 84. Marais waastafu wa Marekani Bill Clinton, George Bush, Barack Obama na Rais wa sasa Joe Biden wamemmiminia sifa bi. Madeleine kwa utumishi wake bora. Katika taarifa, Obama amesema Madeleine alifungua njia za maendeleo katika maeneo mbalimbali ya dunia yaliyokumbwa na migogoro na pia alikuwa bingwa wa maadili ya kidemokrasia. Makao makuu ya Umoja wa Mataifa, ambamo Albright alihudumu kama balozi wa Marekani kutoka mwaka 1993 hadi 1997, yalikaa kimya kwa dakika moja kwa heshima yake. Familia ya Albright imesema alifariki kutokana na ugonjwa wa saratani.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii