Mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi za Kiislamu wameanza mkutano wao leo mjini Islamabad nchini Pakistan.Viongozi wa nchi hizo chini ya muungano wa OIC wanakutana wakiwa na ajenda inayolenga kuidhinisha zaidi ya maazimio 100, ikiwemo msaada wa kifedha kwa Afghanistan na msaada kwa Wapalestina na Kashmir.Mkutano huo pia unahudhuriwa na waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi licha ya Beijing kukosolewa kuhusu matendo yake kwa Waislamu katika mkoa wake wa Xinjiang.Kauli mbiu ya mkutano huo wa OIC ni Kushirikiana kwa Umoja, Haki na Ustawi. Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan anayekabiliwa na changamoto kubwa zaidi dhidi ya utawala wake tangu alipochukua uongozi Agosti 2018, anatarajiwa kutoa hotuba kuu.
Khan anaonekana kupoteza uungwaji mkono wa vyama viwili kongwe vilivyomsaidia kuibuka mshindi na vilevile anaonekana labda kupoteza uungwaji mkono wa jeshi.