Mahakama ya wilaya ya Babati mkoani manyara imemuhukumu mtu mmoja aliefahamika kwa jina Gisgusta Ginanai mwenya umri wa miaka 35 mkazi wa Serengeti mkoani mara kifungo cha miaka 19 kwa kosa la wizi .
Akisoma mashitaka hayo wakili Chris Mgaya amesema mtuhumiwa huyo alitenda makosa hayo July 23 2020 hadi august 18 mwaka 2020 ambapo mtuhumiwa alikutana na mlalamikaji Martine Andrew mwenye umri wa mika 52 nyumbani kwa Amos Baso kijiji cha Abechi kata ya Secheda wilaya ya babati mkoa wa manyara kwa ajili ya matibabu ya kienyeji.
Amesema siku hiyo mlalamikaji mwenye tatizo la kutokuona alimuomba mtuhumiwa huyo amsaidie kuhamisha hela kutoka katika account yake ya benk kwenda kwenya simu ya ke ya mkononi na kisha kumpatia namba za siri na siku zilizo fata mtuhumiwa alimuomba mlalamikaji simu ii aweze kuwapigia ndugu zake na ndipo alipo tumia nafasi hiyo kuhamisha fedha kwenda kwenya account zake tofauti tofauti.
Aidha mlalamikaji baada ya kugundua ameibiwa fedha zake alitoa tarifa katika kituo cha polisi babati na kuanza msako wa mtuhumiwa ambapo alikamatwa mafichoni mpanda mkoani Katavi na kufikishwa mahakamani ili kujibu makosa 19 ya wizi wa kimtandao.