Wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia imesema inakaribisha "kauli chanya" iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Lebanon, katika ishara ya kurudisha uhusiano kati ya Beirut na mataifa ya ghuba ya kiarabu. Katika taarifa, Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati alisisitiza juu ya umuhimu wa kusitisha shughuli zote zinazofanywa na Lebanon zinazoathiri usalama wa Saudi Arabia na mataifa ya ghuba ya kiarabu. Mikati aliongeza kuwa, serikali ya Lebanon imejitolea kuimarisha ushirikiano na Saudi Arabia kufuatia mazungumzo ya simu na Waziri wa mambo ya nje wa Kuwait . Wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia imesema inakaribisha kauli ya Mikati na inatumai kwamba itachangia kuboresha uhusiano wa Lebanon na mataifa mengine ya ghuba ya kiarabu. Mwaka uliopita Saudi Arabia na mataifa ya ghuba ya kiarabu yaliwafukuza mabalozi wa Lebanon katika mzozo wa kidiplomasia uliochangia kwa kiasi kikubwa mgogoro wa kiuchumi nchini Lebanon kufuatia matamshi ya aliyekuwa waziri wa habari George Kordahi kuhusu vita vya Yemen