Wajumbe wa Umoja wa Mabunge Duniani IPU wakiwa katika mkutano wa 144 wa Umoja huo wakisikiliza hotuba mbalimbali za Maspika zikiwasilishwa leo Machi 22, 2022 katika kituo Cha kimataifa Cha Mikutano Bali nchini Indonesia.
Dkt. Joseph Mhagama na Mhe. Esther Matiko wakishiriki kikao cha Baraza la Uongozi la Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) mapema leo Machi 22, 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Bali nchini Indonesia kabla ya Vikao Vya Bunge kuanza. Ambapo wamemchagua Spika wa Baraza la Wawakilishi la Indonesia, Mhe. Puan Mahaaran kuwa Rais wa Mkutano huo wa 144 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).
Vile vile, Baraza hili
limepokea taarifa mbali mbali ikiwemo ya Rais wa Umoja wa Mabunge
Duniani (IPU), Mhe. Duarte Pacheco kuhusu utekelezaji wa majukumu tangu
kumalizika kwa Mkutano wa 143, taarifa ya utekelezaji wa Shughuli za
Bunge kwa kipindi cha Miaka mitano 2017-2021 ambayo imewasilishwa na
Katibu Mkuu wa IPU, Mhe. Martin Chungong, taarifa kuhusu mahali pa
kufanyia Mikutano ya 145, 146 na 147 ya Bunge la Dunia, Mpango Kazi wa
Bunge kwa mwaka 2022/2026.