Ujerumani yalegeza masharti ya kukabiliana na Covid-19

Ujerumani imeondosha mkururo wa mwanzo wa vizuizi vya kukabiliana na vurusi vya corona kitaifa, hatua ambayo imezusha wasiwasi wa kwa taifa hilo linaweza kuendelea kuibuka tena kwa ongezeko la visa vya maambukizi. Kuanzia leo hii, abiria wa treni za kutoka jiji moja kwenda jingine hawatalazimika kuonesha cheti cha uthibitisho wa chanjo, kipimo cha hivi karibuni cha korona au umepona ugonjwa wa Covid-19.Katika maeneo mengi ya kazi kadhalika, waajiri hawatalazimika kuwafanyia ukagauzi wafanyakazi wao kuhusu masharti hayo kabla ya kuingia katika maeneo yao ya kazi kama ilivyokuwa mwanzo.Hata hivyo, masharti mingine kama kuvaa barakoa katika maeneo ya ndani, yataendelea kutumika hadi Aprili 2, pale ambapo majimbo 16 ya Ujerumani yatakapofanya tathimini nyingine baada ya majuma haya mawili ya mwanzo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii