Mkuu wa WHO asema janga kubwa zaidi ya kiafya duniani liko Ethiopia

Wakati ulimwengu unatoa zingatio kubwa kwa mgogoro wa Ukraine, Shirika la Afya Duniani limesema hakuna mahala duniani ambapo afya za watu zipo katika kitisho kibaya zaidi kama jimbo la Tigray, nchini Ethiopia. Mkurugenzi mkuu wa WHO, Adhanom Ghebreyesus amesema hali ilivyo katika jimbo la Tigray ambako yeye ndiko anakotoka, imekuwa mbaya zaidi, kutokana na habari zake za ndani ya jimbo hilo kutofahamika ulimwenguni kwa takribani siku 500 sasa. Hakuna msaada wa vyakula tangu katikati ya Desemba. Akiwaambia waandishi wa habari Tedros aliongeza kwa kusema takribani robo tatu ya vituo vya afya, kwa uchunguzi wa WHO, imebomolewa.Anasema katika eneo hilo hakuna tiba kwa kiasi ya watu 40,000 ambao wanaishi na virusi vya Ukimwi. Mapema mwaka huu serikali ya Ethiopia iliandika barua kwa WHO, wakimtuhumu Tedros kwa utovu wa nidhamu baada ya kutoa maneno ya ukosoaji mkali katika vita na janga la kiutu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii