Wabunge wa Iraq kumchagua rais Machi 26

Bunge la Iraq limeitaja Machi 26 kuwa siku ya uchaguzi wa rais wa taifa hilo, baada ya kucheleweshwa. Aidha limetoa orodha ya mwisho ya wagombea 40.Miongoni mwa wagombea wenye kutajwa kuwa na nafasi kubwa ni pamoja na rais wa sasa Barham Saleh na mpizani wake Reber Ahmed wa chama cha Kikurd cha PUK.Siasa za Iraq zilitumbukia katika misukosuko zaidi baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2021, ambao wapiga kura wachache walijitokea, kulikotokana na ghasia na kucheleweshwa kwa miezi kadhaa, hadi kutolewa matokeo ya mwisho yalipothibitishwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii