Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amealikwa mjini Kiev wakati jiji hilo likiwa katika hatua ya kukaribiwa na hali nyingine ya mashambulizi ya Urusi.Ofisi ya Papa ya mjini Vatican imethithitbitisha kupokea barua hiyo iliyoandikwa Machi 8, kutoka kwa Meya wa Kiev Vitali Klitschko, ikiomba Papa alitembelee jiji hilo au ahudhurie mkutano kwa njia ya video na wakazi wa jiji hilo lililozingirwa.Maneno yalioandikwa katika barua hiyo yanasema ni muhimu kuokoa maisha ya watu na kuweka wazi njia ya amani kwa maisha yao.Vatican haijasema lolote kufuatia barua hiyo lakini kwa mara kadhaa Papa Francis amekuwa akirejea wito wa amani tangu Urusi iivamie Ukraine.