Rais Joe Biden wa Marekani Alahimis ya juma lijalo anatarajiwa kwenda mjini Brussels kwa lengo la kuhudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya ambapo ajenda kuu inatarajiwa kuwa mzozo wa Ukraine.Mkutano huo wa Machi 24 wa kiongozi wa Marekani na washirika wake wa mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya utajadili hatua za mataifa ya Magharibi dhidi ya Urusi.Aidha katika hatua nyingine kupitia ukurasa wake wa Twitter, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami, NATO, Jenerali Jens Stoltenberg ameandika viongozi wa mkutano huo pia ambao utafanyika Machi 24 utajadili uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.Katibu mkuu huyo amesema ameitisha mkutano huo mkubwa wenye shabaha ya kuonesha uungaji wao mkono kwa Ukraine na kuongeza Amerika ya Kaskazini na Ulaya lazima zisimame pamoja.