Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza Dominic jana Jumatatu amesema Uingereza inaunga mkono jitihada ya Mahaka ya Kimatiafa ya ICC katika kuchunguza uhalifu wa kivita nchini Ukraine.Naibu huyo aliwaambia waandishi wa habari mjini The Hague baada ya kukutana na Khan kwamba upo umuhimu wa kuwafikisha ujumbe makanda wa vita wa Ukraine na Urusi kwamba kama watafanya uhalifu wa kivita si kwamba wataishia tu katika kizimba cha The Hague bali pia gerezani. Baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine wa Februari 24, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahaka ya ICC, Karim Khan alisema ameanzisha uchunguzi rasmi uliohusu uwezekano wa kufanyika maouvu katika ardhi ya Ukraine kuanzia 2014, baada ya wanatoaka kujitenga wenye maskani yao nchini Urusi kuteka bandari ya mashariki ya mbali.