Viongozi wa Ujerumani na Uturuki wakutana

Uturuki na Ujerumani zimekubaliana kuendelea kufanya jitihada za kidiplomasia katika kuhakikisha mapigano yanasitishwa nchini Ukraine, huku wakisistiza pia umuhimu wa uhusiano wa pamoja na ushirikiano katika Umoja wa wa Kujihami NATO. Akizungumza katika mkutano wa pamoja na Rais Recep Erdogan, Kansela Olaf Scholz akiwa katika ziara yake ya kwanza Uturuki tangu aingie madarakani alisema kama washirika wa NATO wamethibitisha fikra zao za pamoja na wasiwasi. Erdogan kadhalika aligusia uhusiano wake na Urusi, amboa ulifanikisha kwa taifa lake kuwa mwenyeji wa mkutano wa kidemokrasia wa juma lililopita kati ya Ukraine na Urusi. Tofauti na mataifa ya Ulaya Uturuki haijafunga anga yake kwa ndege za Urusi lakini Erdogan anasema taifa lake limefanya kila lililomuhimu katika kuteleza kanuni za Umoja wa Matiaifa.Katika hatua nyingine Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema mazungumzo kati ya Ukraine na Urusi yataendelea leo. Lakini pia amesema amefanikiwa kuzungumza na Waziri Mkuu wa Israel, Naftali Bennett, ikiwa jitihada ya kuvimaliza vita vinavyoendelea sasa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii