Ujerumani imesema itaziondoa baadhi ya ndege zake za kivita za zamani aina ya Tornado kwa kununua aina mpya kutoka Marekani ya F-35A, zenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia.Akitangaza uamuzi huo Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Christine Lambrecht amesema Ujerumani pia itaboresha ndege zake nyingine Eurofighter Typhoon kwa kufaniklisha vita vya kieletroniki, uwezo ambao kwa sasa unatekelezwa na Tornado. Eurofighter zitaondolewa kuanzia 2040, na mfumo mpya wa makabiliano ya anga (IFCAS),ambao umeboreshwa kwa ushirikiano wa Ufaransa na Uhispania. Kamanda wa jeshi la anga wa Ujerumani, Ingo Gerhartz amesema vita vya sasa vya Ukraine zimesababisha ulazima wa uchaguzi wa ndege hizo za Kimarekani aina ya F-35.