Mkuu wa kamisheni ya haki za binaadamu ya Umoja wa Mataifa, Michelle Bachelet amelaana vikali hukumo ya kifo kwa watu 81 kwa siku moja huko Saudi Arabia. Mkuu huyo amelitaka taifa hilo la kifalme kuacha mara moja kuteleza hukumu ya kifo. Katika taarifa yake kwa umma kiongozi huyo inasema hukumu hiyo ya Juamosi ilitokana na tuhuma zenye kuhusishwa na ugaidi. Hata hivyo katika utetezi wake Saudi Arabia yenye ilisema hukumu hiyo ilitekelezwa kwa misingi ya sheria za taifa hilo kwa maslahi ya usalama wa taifa.