Kalonzo Musyoka "Nitaanza Kampeni Mara Tu Raila Odinga Atakapoapishwa"

Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka amesema atatumia mbinu za Naibu Rais William Ruto iwapo kinara wa ODM Raila Odinga atashinda kiti cha urais kwenye uchaguzi wa Agosti 9.
Kama vile Ruto alivyomfanyia Rais Uhuru Kenyatta, Kalonzo alisema ataanza kampeni zake za urais 2027 mara tu baada ya Waziri Mkuu huyo wa zamani kuapishwa kama rais wa tano.
Akizungumza huko Tharaka Nithi mnamo Jumatatu, Machi 14, Kalonzo alibainisha kuwa Ruto alijua anataka kumrithi Uhuru na alianza kampeni zake 2017 baada ya kiongozi wa taifa kuapishwa kwa muhula uliopita.
"Ruto alijua kuwa anataka kuwa rais kwa hivyo alianza kufanya kampeni mara moja Uhuru alipoapishwa kwa muhula wake wa mwisho. Nimejifunza mengi kutoka kwake. Mara tu Raila atakapokuwa rais, nitaanza kampeni zangu siku inayofuata," Kalonzo alisema.
Inapaswa kukumbuka kuwa Uhuru alimshutumu Ruto kwa kuhujumu serikali yake kwa kuwa hakuwa afisini kutokana na kampeni zake za mapema ambazo rais alisema ziliyumbisha utawala wake.
Katika mkutano wa Sagana State Lodge, kiongozi wa taifa alisema alitofautiana na DP alikuwa na shughuli nyingi za kufanya kampeni kwa gharama ya kuwafanyia kazi Wakenya.
Kalonzo alitangaza kumuunga mkono Raila bila kuyumba katika azma yake ya kuwania urais mnamo Jumamosi, Machi 12.
Makamu huyo wa rais wa zamani hatimaye alijiunga na mrengo wa Azimio La Umoja baada ya misukosuko ambapo alipuuza uwezekano wa yeye kushirikiana na Raila baada ya uchaguzi wa 2013 na 2017

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii