Watu 10 wamepoteza maisha Kaskazini Mashariki mwa nchi ya Guinea wiki hii, baada ya kuzuka kwa mapigano makali kati ya maafisa wa usalama na wachimba dhahabu.
Serikali nchini humo imethibitisha mauaji hayo, yaliyotokea wakati wa operesheni iliyolenga kukomesha uchimbaji haramu wa dhahabu.
Raia watano wa kigeni ni miongoni mwa watu waliouawa kwenye makabiliano hayo, huku watu wengine 13 wakiwemo maafisa wa usalama wakijeruhiwa.
Operesheni hiyo ilikuja baada ya serikali ilikuja baada ya kutumwa kwa wanajeshi katika machimbo yenye utajiri wa dhahabu ya Siguiri siku ya Jumatano, baada ya serikali Novemba tarehe mbili kutangaza marufuku ya wachimbaji wasiokuwa na vibali.
Tangu kuanza kwa opersheni hiyo, maafisa wa usalama wamefanikiwa kuwafukuza maelfu ya raia wa kigeni waliokuwa wamekuja kuchimba madini ya dhahabu katika machimbo hayo, huku maafisa nchini Mali wakisema wamewapokea watu 160,000 waliofukuzwa kutoka Guinea.