Erdogan na Scholz kuijadili Ukaine mjini Ankara

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan atajadili vita nchini Ukraine na Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz katika mazungumzo yatakayofanyika mjini Ankara leo. Uturuki na Ujerumani zinaendeleza juhudi za kupatikana muafaka wa kusitishwa vita ikiwa ni siku 19 tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Uturuki ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO ina mpaka wa baharini na Ukraine na Urusi katika Bahari Nyeusi na ina mahusiano mazuri na nchi zote mbili. Imesema uvamizi huo haukubaliki na kuiunga mkono Ukraine, lakini pia imepinga vikwazo dhidi ya Moscow, wakati ikijitolea kuwa mpatanishi. Ziara ya leo itakuwa ya kwanza ya Scholz nchini Uturuki tangu alipoingia madarakani Desemba 2021 na inafanyika wakati kukiwa na juhudi za Ujerumani kuzungumza na Rais wa Urusi, Vladmir Putin kusitisha uvamizi wake nchini Ukraine. Ujerumani na Ufaransa zipo mstari wa mbele katika Umoja wa Ulaya kuongoza juhudi za kumaliza vita hivyo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii