Mazungumzo ya Chad yaanza kwa kugonga mwamba Doha

Serikali ya kijeshi ya Chad na makundi kadhaa ya upinzani walianza mazungumzo ya amani jana nchini Qatar kama hatua ya kwanza kuelekea kuumaliza uasi na kuandaa uchaguzi. Lakini baada ya hotuba za ufunguzi, ambapo waziri mkuu wa nchi hiyo na mkuu wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika walihimiza makubaliano, mazungumzo hayo yalisitishwa kwa saa 48 kwa sababu ya mzozo kuhusu muundo wake. Karibu makundi 44 ya waasi na upinzani yalialikwa kwenye mkutano huo wa Doha. Chama kikuu cha upinzani cha Front for Change and Concord nchini Chad - FACT na washirika wake kadhaa walikataa kuanza mazungumzo rasmi baada ya hotuba za ufunguzi. Msemaji wa FACT Issa Ahmat, amesema upinzani hautaki mazungumzo ya moja kwa moja na wawikilishi wa serikali na unataka Qatar iwe mpatanishi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii