Kimbunga Gombe chaua watu wasiopungua 10 Msumbiji

Idara ya Usimamizi wa Majanga nchini Msumbiji imesema jana kuwa watu wasiopungua 10 wameuawa na kimbunga Gombe kilichotua kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo. Idara hiyo imesema pia kuwa zaidi ya nyumba 2,200 zimeharibiwa na madarasa 47 katika shule nane yameharibiwa na dhoruba hiyo lililopiga mkoa wa pwani wa Nampula siku ya Ijumaa. Kwa mujibu wa maafisa nchini humo, wilaya sita zilikatiwa kabisaa mawasiliano na ulimwengu wa nje kufikia Ijumaa Mchana. Siku moja kabla, nchi hiyo ilishuhudia mvua kubwa na upepo wenye kasi ya karibu kilomita 200 kwa saa. Eneo la kusini mwa Afrika hivi sasa limo katika msimu wake wa kiangazi wa vimbunga, ambao unaweza kuleta mvua kubwa na dhoruba hadi mwishoni mwa mwezi Aprili.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii