Mkuu wa usalama wa Iran akutana na kiongozi wa kiroho Mojtaba Khamenei

Mkuu wa usalama wa Iran Mohsen Rezaei, Jumanne ya wiki hii, alikutana na kiongozi wa juu wa kiroho nchini humo Ayatollah Mojtaba Khamenei, ambaye hajaonekana hadharani tangu kuuawa kwa babake yake mwezi Machi, mkutano wao ukifanyika ikiwa imepita siku moja tangu Tehran kushiriki mazungumzo na wawakilishi wa Saudi Arabia, Uturuki Pakistan.

Kwa mujibu wa shirika la Habari linalomilikiwa na serikali ya Iran, Khamenei alisisitiza umuhimu kwa kuweka mbele masuala ya yanayoihusu Iran na marsharti ya nchi hiyo kumaliza vita.

Maofisa wa ngazi ya juu kutoka nchini Saudi Arabia, Uturuki na Pakistan walizuru Tehran Jumatatu (Oktoba 26) kwa lengo na kujaribu kupunguza mzozo wa Mashariki ya kati, mzozo ulioanza mwezi Februari baada ya Marekani na Israeli kuishambulia Iran.

Shirika hilo la Habari aidha limeeleza kwamba mkutano kati ya mkuu wa usalama wa Iran na  kiongozi wao wa kiroho uliangazia umuhimu wa kutetea usalama wa Iran na ule wa nchi za ukanda.

Walijadili pia suala la Iran kudhibiti mlango wa Bahari wa Hormuz pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa Jirani katika Ukanda wa mashariki ya kati.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii