Raia wa Israeli wanasubiri matokeo ya uchaguzi mkuu wa Jumanne

Wananchi wa Israeli wanasubiri matokeo ya mwisho ya uchaguzi mkuu uliofanyika jana, huku ripoti zikionesha kuwa, kuna ushindani mkali kati ya muungano wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na mpinzani wake mkuu Gadi Eisenkot.

Baada ya zoezi la upigaji kura kumalizika, Netanyahu na Eisenkot wote wanasema, wana matumaini makubwa ya miungano yao kuibuka na ushindi, wakati huu matokeo yanapoendelea kusubiriwa.

Netanyahu amesema, ana matumaini makubwa kuwa serikali mpya inayoungwa mkono na vyama vya siasa vya mrengo wa kulia itaundwa.

Mpinzani wake Eisenkot naye anayeongoza chama cha Yashar, amesema wapiga kura wameamua kumwondoa Netanyahu madarakani na wanataka mabadiliko.

Matokeo yanapoanza kutangazwa, ripoti zinaonesha kuwa chama cha Likud chake Netanyahu, huenda kikapata viti vingi bungeni, lakini hakuna muungano utakaopata viti 61 vinatakiwa kuunda serikali pekee yake. Viti 120 vya ubunge vinawania kwenye uchaguzi huu.

Kamati hii ilifikia maazimio kuwa, mateso yakukuwa makali, yalikosa ubinadamu,na kusababisha madhara ambayo yangeweza kuzuiwa. Kamati inasisitiza kuwa janga hili lingezuiwa kabisa, na lilisabisha na mzingira magulu ya kuwepo kwa msongano, kutokuwepo kwa watu waliojali, kupuza tahadhari , kutochunguza kilichokuwa kinaendelea  na changamoto za hali ya hewa

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii