Rais Luiz Inacio Lula da Silva ameshinda uchaguzi wa urais

Nchini Brazil, rais Luiz Inacio Lula da Silva, ameshinda uchaguzi wa urais, baada ya kumshindani mpinzani wake wa karibu, katika kinyanganyiro kilichokuwa na ushindani mkali.

Rais Lula da Silva mwanasiasa wa siasa za mrengo wa kushoto, ambaye anatimiza umri wa miaka 81 siku ya Jumanne, amepata ushindi wa asilimia 51.7 na kumshinda mpinzani wake Seneta Flavio Bolsonaro, alieyapata asilimia 48.2.

Ushindi huu wa Da Sila, unamanaisha kuwa ataongoza Brazil kwa muhula wa nne. Hata hivyo, Flavio Bolsonaro mwanasiasa wa siasa za mrengo wa kulia, mtoto wa kiume wa zamani wa zamani Jair Bolsonaro, amekataa kukubali kushindwa, na kutaka matokeo hayo kufutwa.

Uchaguzi huo uliofanyika siku ya Jumapili, uliokumbwa na sintofahamu baada ya Mahakama ya Juu, kuamua kuwa zoezi la upigaji kura liendelee katika baadhi ya maeneo kwa saa mbili, licha ya vituo vya kupigia kura kufungwa.

Wakati Bolsonaro, akipanga kwenda Mahakama kuomba kufutwa kwa  matokeo hayo, da Silva na wafuasi wake, wameendelea kusherehekea, akisema ushindi wake unamaanisha uongo ulishindwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii