Wizara ya afya ya Tanzania imezindua zoezi la utoaji chanjo ya homa ya manjano baada ya mlipuko wa ugonjwa huo kuripotiwa katika nchi jirani ya Kenya.
Waziri Ummy Mwalimu amewaagiza watendaji wa hospitali ya rufaa ya mkoa kuanza kutoa chanjo kwa wale wote wanaosafiri nje ya nchi.
Waziri Mwalimu amewaagiza wataalam wanaosimamia masuala ya afya mipakani kuangalia uwezekano wa kutoa vyeti vya chanjo ya kielektroniki ili kukabiliana na changamoto ya vyeti feki.
Pia ametoa wito kwa watanzania kuchukua tahadhari ili ugonjwa huo usiingie nchini na kuhakikisha mazingira yanakuwa safi ili kuzuia mbu kuzaana