Rubani mkuu na raia wa India Smit Machchhar ambayealichomwa kisu na rubani msaidizi katika tukio la ndege ya flydubai amepongezwa kwa uajsiri wake wa kuzuia janga kubwa.
Rubani mkuu wa ndege ya shirika la Flydubai, Capt. Smit Machchhar, ameendelea kupongezwa na viongozi wa Israel na India kwa mchango wake katika kuzuia maafa baada ya kuzuka kwa tukio hatari akiwa angani. Kwa mujibu wa Ubalozi wa India nchini Saudi Arabia, Machchhar yuko katika hali nzuri na imara, ingawa alijeruhiwa wakati wa tukio hilo. Hata hivyo, mamlaka hazijatoa taarifa kuhusu hali ya afya ya rubani msaidizi aliyekamatwa.
Machchhar, ambaye ana zaidi ya miaka 30 na uzoefu wa zaidi ya muongo mmoja katika urubani, anaripotiwa kuendelea kuidhibiti ndege hiyo licha ya kujeruhiwa. Kitendo hicho kinatajwa kuwa kilisaidia kuzuia ajali ambayo ingeweza kusababisha vifo vya mamia ya watu.
Marafiki na majirani wa familia yake mjini Mumbai wamemuelezea kama mtu mtulivu, mwenye moyo wa kusaidia na ambaye daima hubaki makini hata katika mazingira yenye shinikizo kubwa.
Rais wa India Droupadi Murmu amesema taifa hilo linajivunia hatua za rubani huyo, akimsifu kwa ujasiri na uwezo wa kufanya maamuzi muhimu katika wakati wa hatari. Naye Waziri Mkuu Narendra Modi amesema licha ya kujeruhiwa na kukabiliwa na tishio kubwa, Machchhar alionyesha dhamira ya kipekee ya kuokoa maisha ya abiria.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amempongeza rubani huyo na kusema hatua zake zilisaidia kuzuia janga kubwa.