Addis Ababa inashutumu Asmara, Khartoum, na Cairo kwa kuwaunga mkono waasi wa Tigray

Mapigano yanaendelea nchini Ethiopia. Siku nane baada ya shambulio kubwa kuanzishwa na muungano wa makundi kadhaa ya upinzani yenye silaha kaskazini mwa nchi, mapigano yanaendelea nchini Ethiopia, na kusababisha vifo vingi vya raia. Addis Ababa, kwa upande wake, inashutumu Eritrea, Sudan, na Misri kwa kuwaunga mkono waasi wa jimbo la Tigray.

Nchini Ethiopia, mapigano kati ya jeshi la shirikisho na makundi yenye silaha ya muungano wa upinzani ulioundwa hivi karibuni yanaendelea katika pande kadhaa kaskazini mwa nchi. Na zaidi ya wiki moja baada ya kuanza kwa mashambulizi ya waasi, raia ndi wanaathirika zaidi.

Katika taarifa, shirika lisilo la kiserikali la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limeelezea wasiwasi kuhusu athari ya mgogoro huo kwa raia wa Tigray, ambapo hospitali zimejaa, anaripoti mwandishi wetu huko Addis Ababa, Marlène Panara. Ingawa majeruhi 420 walitibiwa wiki iliyopita huko Korem na Alamata, miji miwili kusini mwa mkoa huo, mbali kidogo mashariki, hospitali huko Shire ilipokea zaidi ya majeruhi 300 mnamo Septemba 25 pekee - takwimu ambazo, kulingana na MSF, zinajumuisha wagonjwa waliotibiwa katika vituo ambavyo ni washirika wao.

Kuhusu hospitali ya Mekele, mji mkuu wa Tigray, iliwapokea raia 44 - wakiwemo watoto 33 - waliojeruhiwa vibaya na mashambulizi na milipuko katika miji mingine katika eneo hilo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii