Mapigano yanayoendelea nchini Ethiopia yazua wasiwasi

Nchini Ethiopia, wakati huu vita vikiendelea kati ya makundi yenye silaha na wanajeshi wa serikali katika jimbo la Tigray, Kamati inayotoa tuzo ya amani ya Nobel, iliyompa ushindi Waziri Mkuu Abiy Ahmed mwaka 2019, inatiwa wasiwasi na kuendelea kwa vita hivyo.

Katibu wa Kamati hiyo ya Nobel, Kristian Harpviken, amesema tangu mwaka 2020 hali ya Ethiopia imeendelea kuzua wasiwasi mkubwa kuhusu amani na usalama wa raia wa nchi hiyo ya pembe ya Afrika.

Mwaka 2019, Waziri Mkuu Abiy alipata tuzo hiyo kutokana na jitihada zake za kufanikisha maridhiano kati ya nchi yake ya Ethiopia na Eritrea, baada ya vita vya zaidi ya miaka 20, lakini vita vinavyoendelea tangu mwaka 2020 sasa vinachafua jina lake kama mtu mwenye amani.

Naye kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo wa 14 ametoa wito kwa makundi yenye silaha na serikali ya Ethiopia, kuwa na mazungumzo ili kumaliza vita vinavyoendelea.

Vita vilianza wiki iliyopita na kuzua wasiwasi wa kushuhudiwa kwa mauaji makubwa kama iivyoshuhudiwa kati yam waka 2020 hadi 2022 wakati watu 600,000, walipopteza maisha na mamilioni kuyakimbia makaaazi yao.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii