Mabaki ya Binadamu yagunduliwa katika misitu ya jimbo la Abia

Ugunduzi wa kutisha umefanywa kusini mashariki mwa Nigeria. Mabaki ya binadamu yalipatikana Jumamosi, Septemba 26, na polisi katika misitu kadhaa katika Jimbo la Abia, ambapo wahalifu wanajulikana kujificha. Mifupa hii inaweza kuwa ya waathiriwa wa utekaji nyara. Shirika la Amnesty International Nigeria limeitaka serikali kuchukua hatua ili kuhakikisha haki kwa familia za waathiriwa.

Mafuvu na mifupa ilikuwa haijafichwa vizuri kwenye uoto wa asili, vidio iliyotolewa na jeshi la polisi la jimbo inafunua. Ilirekodiwa wakati vikosi kadhaa vya usalama vikiendesha operesheni ya kuwatimua wahalifu waliokuwa wamekimbilia katika misitu ya eneo hilo.

Kulingana na taarifa za polisi, mafuvu na mifupa haya 28 yanaweza kuwa ya waathiriwa wa utekaji nyara, ingawa haijulikani haswa ni lini vifo hivyo vilitokea. Hakuna mtu yeyote aliyekamatwa: washukiwa walitoroka wakati polisi na vikosi maalumu walipowasili.

Eneo linachunguzwa

Msemaji wa polisi wa eneo hilo Maureen Chioma Chinaka amesema kwamba uchunguzi unaendelea na kwamba eneo hilo bado linachunguzwa, kwa matumaini ya kuwakamata washukiwa. Ingawa eneo la kusini-mashariki mwa nchi linachukuliwa kuwa salama kiasi kutokana na utekaji nyara wa kudai fidia, ikilinganishwa na maeneo mengine ya Nigeria, bado vitendo hivyo vinafanyika huko."

Katika taarifa, Amnesty International Nigeria imeiwasihi mamlaka kuchunguza na kuwafikisha mahakamani wale waliohusika na unyanyasaji huu ili haki iweze kutolewa kwa familia za waathiriwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii