Waandishi wa habari wa Ufaransa na msaidizi wao wameachiliwa huru kwa muda

Nchini Togo, waandishi hao wawili wa habari wa Ufaransa na msadizi wao, raia wa Togo, ambao walikuwa wamefungwa kwa wiki kadhaa huko Lomé, wako huru. 

Wanahabari wawili wa Ufaransa Gaël Mocaër na Sebastian Perez Pezzani pamoja na msaidizi wao, raia wa Togo Fred Vedomey, walikamatwa nchini Togo na hatimaye kuachiliwa kwa muda mnamo Septemba 1, 2026.

Mnamo Jumanne, Septemba 1, walinufaika na uamuzi wa mamlaka ya mahakama ya Togo wa kuwapa uhuru wa muda. "Kuzuiliwa kwao kizuizini hakuhitajiki tena kwa ajili ya kubainisha ukweli," mmoja wa mawakili wao aliiambia RFI. Gaël Mocaër na Sebastian Perez Pezzani, ambao walisafiri kwenda Togo kukirekodi sehemu ya kipindi cha makala ya televisheni inayoitwa "Les Routes de l'impossible" (barabaraza zisizowezekana), mfululizo wa makala unaorushwa kwenye Televisheni ya Ufaransa ya France Télévisions. Walikamatwa mnamo Julai 27 kaskazini mwa Togo pamoja na msaidizi wao Fred Vedomey. Wanashtakiwa kwa kutoa taarifa za uongo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii