Ujerumani yarekodi maambukizi mapya ya COVID-19 .

Maambukizi ya virusi vya corona nchini Ujerumani yamepindukia watu laki mbili na elfu hamsini (250,000) kwa siku moja kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa janga hilo. Haya ni kwa mujibu wa taasisi ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza Ujerumani, Robert Koch. Taasisi hiyo imeripoti vifo vya watu 259 siku ya Jumatano. Wataalam wamesema idadi ya maambukizo inaweza kuwa kubwa zaidi kwani vituo vingi vya upimaji vilikuwa vikifanya kazi kwa uwezo mdogo.Tangu kuanza kwa janga la corona, watu milioni 16.5 nchini Ujerumani wameambukizwa na wengine zaidi ya laki moja na elfu ishirini na tato wamekufa kutokana na virusi hivyo. Huko Hong Kong mamlaka ya afya imeripoti visa vipya 31,402 vya COVID-19, ambapo visa 7,012 vilithibitishwa kupitia jukwaa la kujiripoti ambapo wakaazi wanaweza kurekosi matokeo ya vipimo vyao.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii