Zelensky aripoti vifo kufuatia mashambulizi ya Urusi Saa 2 zilizopitaSaa 2 zilizopita

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema watu kadhaa wameuawa na wengine wamejeruhiwa katika mashambulizi ya droni za Urusi.

Rais Zelensky amearifu kupitia mtandao wa X kwamba watu wanne wamekufa katika mikoa ya Odesa na Zaporizhzhya baada ya Urusi kushambulia usiku mzima wa jana na watu kumi wamejeruhiwa.

Kwa ujumla, Urusi ilifyatua droni 130 na makombora manane, hii ikiwa ni kulingana na kiongozi huyo.

Wakati huohuo, mkuu wa vikosi vya droni nchini Ukraine, Robert Brovdi, ameripoti kuzishambulia meli nyingine 12 za Urusi katika Bahari Nyeusi tisa za mizigo, meli moja ya mafuta, moja ya kusafirisha gesi, na boti moja ya kuvuta meli.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii