watu 11 wamefariki na wengine 19 wamejeruhiwa katika kisa cha moto, ambao bado unawaka, katika kituo cha watoto yatima katika viunga vya Algiers,Polisi jamii ya Algeria imetangaza mnamo Julai 16, 2026, bila kutaja umri wa waathiriwa.
Polisi jamii ya Algeria imeripoti leo Alhamisi kwamba moto uliozuka katika kituo cha watoto yatima katika manispaa ya Mohammadia, kinachopatikana katika viunga vya Algiers, umesababisha vifo vya watu wasiopungua 11 na 19 kujeruhiwa. Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.
"Polisi jamii inaendelea na shughuli za kuzima moto uliozuka katika kituo cha watoto mayatima, kinachopatikana katika manispaa ya Mohammadia," Polisi jamii imesema katika taarifa kwa vyombo vya habari. "Idadi ya vifo kwa sasa ni 11," taarifa hiyo imeongeza.
Waziri Mkuu Sifi Ghrieb amewatembelea majeruhi katika kitengo cha moto cha Zeralda katika vitongoji vya Algiers, na kisha katika hospitali ya Mustapha Bacha katika mji mkuu, kulingana na televisheni ya taifa.
Nchi imekuwa ikipitia wimbi la joto la kipekee kwa siku kadhaa, na karibu matukio ya elfu moja ya moto yamerekodiwa katika wiki iliyopita.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime