Bunge la Ukraine linatarajiwa hivi leo kuipitisha serikali mpya ya wakati wa vita, baada ya rais Volodymyr Zelensky kufanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.
Mabadiliko haya ambayo ni ya pili ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, yameibua hasira ya umma iliyoshuhudia maelfu wakiandamana hasa wakipinga uamuzi wa kuondolewa kwa waziri wa ulinzi Mykhailo Fedorov hasa wakati huu nchi hiyo ikikabiliana vikali na Urusi.
Fedorov mwenye umri wa miaka 35 ambaye nafasi yake itachukuliwa na waziri wa Mambo ya Ndani Ihor Klymenko, ni mtaalamu wa teknolojia na aliapa kufanya mageuzi makubwa ndani ya jeshi la Ukraine ili kuwa na kikosi chenye ufanisi zaidi.
Hayo yanajiri wakati Urusi na Ukraine zimeendelea kushambuliana vikali usiku wa kuamkia Alhamisi, huku pande zote zikilenga miundombinu ya nishati, bandari na meli za mafuta katika maeneo mbalimbali. Watu wawili wameuawa Kiev na mmoja huko Urusi katika mkoa wa Bryansk.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime