Majaribio ya dawa na chanjo dhidi ya mlipuko wa Ebola yameanza ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukabiliana na kudhibiti ugonjwa huo katika taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Shirika la Afya Duniani, WHO limesema licha ya dalili za matumaini baada ya majaribio ya awali, itachukua miezi kadhaa kabla ya dawa au chanjo hizo kupatikana kwa matumizi ya watu wengi. Kufikia sasa wagonjwa 50 wameandikishwa kuwa sehemu ya jaribio la kwanza la dawa, katika vituo vitatu vya matibabu.
Uingereza, Canada zafanya majaribio ya chanjo
Wakati huo huo, majaribio ya chanjo yameanza nchini Uingereza na Kanada ili kutathmini mwitikio wa kinga ya mwili. Hadi sasa, hakuna chanjo iliyoidhinishwa kwa virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo, ambayo imeshasababisha vifo vya takriban watu 1,700 nchini Kongo.