Watu wanne, wakiwemo raia watatu, wameuawa na mwanajeshi mmoja huko Sevastopol, gavana wa eneo hilo kwenye pwani ya Bahari Nyeusi katika eneo la Crimea lililounganishwa na Urusi amesema leo Jumanne, Agosti 4.
"Tukio mbaya limetokea huko Sevastopol (...). Kulingana na ripoti za awali, mwanajeshi mmoja aliwafyatulia risasi wanajeshi wenzake, na kumuua mtu mmoja, kabla ya kuwashambulia raia na kuwaua watatu," Mikhail Razvojaev aliandika kwenye Telegram. Alisema kwamba tukio hilo lilitokea katika wilaya ya Khmelnitskoye ya Sevastopol.
Miongoni mwa waathiriwa ni wanaume wawili wenye umri wa miaka 71 na 59, pamoja na mwanamke mwenye umri wa miaka 64, Mikhail Razvojaev ameongeza.