Salah Kutua Uturuki leo

Klabu ya Trabzonspor ya Uturuki imethibitisha kuwa ipo kwenye mazungumzo ya kumsajili nyota wa Misri, Mohamed Salah, huku ikitangaza kuwa mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili Istanbul leo, Jumatano Agosti 5, 2026, kwa ajili ya mazungumzo ya mwisho kuhusu uhamisho wake.

Katika taarifa yake, Trabzonspor ilisema Salah atawasili Uwanja wa Ndege wa Ataturk jijini Istanbul kabla ya kuelekea Trabzon baadaye siku hiyo ikiwa sehemu ya mchakato wa kukamilisha usajili wake.

Salah, mwenye umri wa miaka 34, aliondoka Liverpool mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka tisa yenye mafanikio makubwa. Akiwa Anfield, alishinda taji la UEFA Champions League, mataji mawili ya Ligi Kuu England na kuweka rekodi ya kufunga mabao 257 katika mechi 442, na kuwa mfungaji wa tatu bora katika historia ya Liverpool.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii