Ngorongoro Heroes imefuzu kucheza Fainali

Timu ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa

miaka 20 (Ngorongoro Heroes) imefuzu kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana (U-20 AFCON) zitakazofanyika nchini

Ghana, ikiongozana na timu ya taita ya Sudan kutoka ukanda wa

Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Tanzania imekata tiketi hiyo baada ya kuichapa Burundi mabao 2-0 kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Mabao ya ushindi yalifungwa na Juma Abushiri na Faraji Kayanda.

Sudan imefuzu AFCON kufuatia ushindi mabao 3-2 dhidi ya Uganda

katika mchezo mkali wa nusu fainali ya kwanza.

Mchezo wa fainali wa CECAFA U-20 kati ya Tanzania na Sudan utachezwa siku ya Alhamis, Septemba 24, 2026 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii