Kiongozi wa upinzani Uganda ni dhaifu sana hospitalini

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye, ambaye anakabiliwa na kesi ya uhaini, ana fahamu lakini "hali yake ni dhaifu sana" na hawezi kuzungumza.

Akizungumza nje ya hospitali ya Mulago jijini Kampala alikolazwa mumewe, Byanyima ambaye ni Mkuruzengi Mkuu wa shirika la UNAIDS, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mumewe hawezi kuzungumza wala kuandika kwa sababu mikono yake haina nguvu.

Besigye, mwenye umri wa miaka 70, mpinzani wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni, amekuwa gerezani tangu mwishoni mwa mwaka 2024 alipotekwa nyara nchini Kenya na kurudishwa Uganda kwa njia ya kisiri.

Besigye alilazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi katika mji mkuu wa Uganda, Kampala, baada ya kuzimia wakati wa kikao cha mahakama mnamo Julai 30. Alianguka muda mfupi baada ya kukemea uamuzi wa mahakama wa kuteua mawakili wa kumwakilisha. Wakili wake mkuu wa utetezi, Erik Lukwago, alikamatwa, huku waziri wa zamani wa sheria wa Kenya Martha Karua, mwanachama mwingine wa timu yake ya mawakili, akizuiliwa kuingia Uganda. Alisema haki za Besigye za kuishi, kupata huduma sahihi za matibabu na kesi yake kuendeshwa kwa njia ya haki lazima ziheshimiwe, akisema kuwa "zinapuuzwa".

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii