Mrembo mmoja raia wa Zambia mwenye umri wa miaka 24, anayejulikana kwa jina Teresia, amefichua kuwa yeye huchumbiana na wanaume wote ambao hugharamia maisha yake ya kifahari.
Teresia alisema huwatosheleza wanaume hao wote kingono na huvuna zaidi ya shilingi TSh milioni 1,200,000 kutoka kwa kila mmoja wao na ameweka kwa mtu yeyote ambaye anachumbiana naye au anayetaka kumchumbia.Binti huyo mwenye umri wa miaka 24, alifichua kuwa kwa sasa yuko katika mahusiano ya kimapenzi na wanaume sita ambao wameoa.
Teresia alisema kuwa wanaume wenyewe ndio humtafuta na yeye hawatafuti na alipoulizwa umri wa wapenzi wake alisema ni kuanzia miaka 53.
“Usiwahi kufikiria kuibua suala la ndoa kama wewe ni mvulana. Waachie watu walio na msimamo wa kifedha na waliokomaa. Itakuvunja. Unaweza kuingia kwenye ndoa ukidhani anakupenda. Hii ni moja ya sababu kwa nini kuna visa vingi vya talaka kwa sababu ndoa imekiukwa,” alisema.