Wakimbizi wa Ukraine kufikia milioni 2 leo au kesho: UN

Idadi ya wakimbizi wanaokimbia vita nchini Ukraine inatarajiwa kufika milioni mbili katika siku mbili zijazo. Mkuu wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa Filippo Grandi amesema leo mjini Oslo kuwa idadi hiyo itaongezeka hata zaidi kama vita vya Ukraine havitakomeshwa. Hapo jana, UNHCR ilisema idadi ya wakimbizi waliokimbia Ukraine ilikuwa milioni 1.7. Grandi ametoa kauli hizo katika kikao cha waandishi wa habari baada ya kuzuru Moldova, Poland na Romania, nchi ambazo zimewapokea wakimbizi wanaomiminika mpakani kutokea Ukraine tangu Urusi ilipovamia nchi hiyo Februari 24. Kwa ulinganisho, Grandi amesema katika vita vya Balkan nchini Bosnia na Kosovo kulikuwa na karibu watu milioni mbili hadi tatu waliokimbia lakini idadi hiyo ilikuwa katika kipindi cha miaka minane.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii