Mapigano makali yatikisa Mogadishu

Mapigano yametikisa Mogadishu usiku kucha huku vikosi vya usalama vikikabiliana na wanamgambo waliovamia maeneo kadhaa.

Milio ya risasi imetikisa mji mkuu wa Somalia Mogadishu usiku kucha wakati wa mapigano makali kati ya makundi ya kisiasa kabla ya maandamano yaliyopangwa leo.

Kwa mujibu wa polisi wanajeshi wanaendesha operesheni kubwa ya kiusalama dhidi ya wanamgambo wenye silaha nzito walioshambulia baadhi ya maeneo kwa mabomu ya kurusha.

Mapigano hayo yalizuka wakati viongozi wa upinzani walipowasili mjini Mogadishu kushiriki maandamano dhidi ya uamuzi wa Rais Hassan Sheikh Mohamud kuongeza muda wa uongozi wake kwa mwaka mmoja.

Hata hivyo rais Mohamud anasema mabadiliko ya katiba yanampa muda wa ziada lakini hali ya kisiasa nchini Somalia bado ni ya wasiwasi mkubwa kutokana na mgawanyiko wa makundi ya kisiasa na tishio la kundi la Al-Shabaab.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii