Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa atahudhuria mkutano wa G7 utakaofanyika Ufaransa katikati ya mwezi Juni.
Trump atasafiri kwenda Ufaransa mara baada ya tamasha la mapigano ya sanaa za kijeshi (UFC) litakalofanyika katika Ikulu ya Marekani (White House) kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa ya miaka 80 tarehe 14 Juni. Haya ameyandika kwenye mtandao wake wa Truth Social siku ya Jumatano. Kundi la mataifa yenye nguvu kiuchumi linajumuisha Marekani, Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Italia, Canada na Japan, pamoja na Umoja wa Ulaya. Kundi hilo litakutana kuanzia tarehe 15 hadi 17 Juni. Canada ndiyo iliyokuwa mwenyeji wa mkutano wa G7 mwaka uliopita.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime