Algeria iliwashangaza Uholanzi kwa kuwafunga bao 1-0 mjini Rotterdam hapo Juni 03,2026 katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na Kombe la Dunia wiki moja kabla ya mashindano ya mwaka 2026 kuanza huko Kaskazini mwa Amerika.
Kinyume na matarajio bao zuri lililofungwa dakika ya 86 na Hadj Moussa kwa shuti la mguu wa kushoto lililopinda na kuingia juu ya kona liliihakikishia Algeria ushindi katika mchezo ambao kwa kiasi kikubwa ulidhibitiwa na Uholanzi.
Uholanzi walizuiwa mara kwa mara na kipa wa Algeria Luca Zidane, mwana wa gwiji wa zamani wa Ufaransa, Zinedine Zidane kipa huyo mwenye umri wa miaka 28, anayecheza katika klabu ya Granada ya daraja la pili nchini Hispania, ameongeza nafasi yake ya kujumuishwa katika kikosi cha mwisho baada ya Algeriakutaja makipa wanne katika kikosi cha awali, huku watatu tu wakitarajiwa kwenda Kombe la Dunia litakalofanyika Amerika Kaskazini kuanzia tarehe 11 Juni hadi 19 Julai.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime