Ujerumani yapata pigo baada ya kushindwa kuingia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikizidiwa na Ureno na Austria serikali ya Merz yakabiliwa na maswali kuhusu diplomasia yake.
Katika uchaguzi uliofanyika jana Jumatano nchi hiyo ilishindwa na Ureno na Austria ambazo zilipata kura za kutosha kujiunga na baraza hilo kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwakani.
Ujerumani ilipata kura 104 pekee chini ya kura 127 zilizohitajika kushinda hii ni mara ya kwanza kwa nchi hiyo kushindwa katika uchaguzi wa kuwania nafasi kwenye Baraza la Usalama, ambapo imewahi kuhudumu mara sita.
Matokeo hayo yanachukuliwa kuwa pigo kwa serikali ya Kansela Friedrich Merz ambaye amekuwa akitaka kuimarisha nafasi ya Ujerumani katika masuala ya kimataifa Merz amesema nchi yake itaendelea kutekeleza wajibu wake ndani ya Umoja wa Mataifa licha ya kushindwa huko.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann Wadephul amesema Ujerumani ilikuwa tayari kutoa "mchango mkubwa” katika kazi za Baraza la Usalama.
Baraza la Usalama lina jukumu la kusimamia amani na usalama wa dunia na linajumuisha wanachama 15 wakiwemo watano wa kudumu wenye haki ya kura ya turufu.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime