Samia akutana na Putin katika ziara ya siku tatu Urusi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ameanza ziara ya siku tatu nchini Urusi ambako amekutana na Rais Vladimir Putin.

Ziara hiyo inafanyika wakati Tanzania ikikabiliwa na ukosoaji kutoka mataifa ya Magharibi na mashirika ya haki za binadamu kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu baada ya uchaguzi wa mwaka jana.

Katika mazungumzo yao mjini Moscow Dkt. Samia ameitaja ziara hiyo kuwa ya kihistoria huku Putin akisisitiza umuhimu wa kuimarisha biashara kati ya nchi hizo mbili.

Kwa sasa biashara kati aya Tanzania na Urusi ni zaidi ya dola milioni 300 kwa mwaka na mradi pekee wa pamoja ni mgodi wa urani uliopangwa kuanzishwa kwa zaidi ya muongo mmoja.

Aidha ziara hiyo ni ya kwanza ya rais wa Tanzania nchini tangu ziara ya Baba wa Taifa Julius Nyerere, mwaka 1969.

Hata hivyo wachambuzi wanasema Urusi inanufaika kisiasa kwa kuimarisha uhusiano na Tanzania wakati serikali ya Samia ikikabiliwa na shinikizo la kimataifa.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii