WHO yaonya kuwa mlipuko wa Ebola DRC haujadhibitiwa

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, ameonya kuwa mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bado haujadhibitiwa.

Akizungumza baada ya kutembelea eneo lililoathiriwa mashariki mwa nchi hiyo, amesema ugonjwa huo ulianza kusambaa kwa muda kabla ya kugunduliwa katikati ya mwezi Mei. WHO imeripoti jumla ya wagonjwa 344 waliothibitishwa, wakiwemo watu 60 waliopoteza maisha, huku nchi jirani ya Uganda ikithibitisha visa 15. Hata hivyo, changamoto kubwa bado ipo katika kuwafuatilia watu waliogusana na waathirika, pamoja na kukosa imani miongoni mwa jamii, jambo linalochelewesha kudhibiti maambukizi. WHO imesema inaendelea kuongeza uwezo wa upimaji na kuharakisha juhudi za kutafuta chanjo na tiba.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii