Wabunge wa Marekani waidhinisha azimio la kuagiza kukomeshwa kwa vita vya Iran

Baraza la Wawakilishi la Marekani limepitisha azimio siku ya Jumatano linaloamuru kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani katika vita dhidi ya Iran, pigo kwa Donald Trump, ambaye aliingiza Marekani kwenye mzozo huo mnamo Februari 28. Azimio hilo - lililopitishwa kwa kura za wabunge wanne wa Republican - hata hivyo, kimsingi lina umuhimu wa kiishara, kutokana na nguvu ya kura ya turufu ya rais wa Marekani.

Wabunge wa Republican Thomas Massie, Brian Fitzpatrick, Tom Barrett na Warren Davidson waliungana na Democrats kuunga mkono azimio hilo. Barrett alisema ni jukumu la Bunge pekee kutangaza vita na kwamba alipiga kura kulingana na dhamiri yake, bila kujali shinikizo lolote la kisiasa.

Azimio hilo lilipitishwa kwa kura 215 dhidi ya 208, baada ya wabunge wanne wa Chama anachotoka Trump cha Republican kuungana na wale wa Democrats katika hatua ya nadra ya kupinga hadharani vita hivyo, kati ya Marekani na Iran vilivyoanza mwezi Februari.

Hata hivyo, azimio hilo bado linahitaji kupitishwa na Bunge la Senate, linalodhibitiwa na chama cha Republican.

Hata kama azimio hilo linaweza likapitishwa, Trump anaweza kutumia mamlaka yake ya kura ya veto kuzuia azimio hilo kuwa sheria, jambo ambalo linahitaji theluthi mbili ya kura katika mabunge yote mawili ili kubatilishwa.

Licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano, Marekani na Iran zimeendelea kushambuliana katika siku za karibuni

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii