Wachezaji Geita Gold FC wapongezwa

Licha ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Young Africans katika mchezo wa Mzunguuko wa 17 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Wachezaji wa Geita Gold FC wamepongezwa na Uongozi wa klabu hiyo.

Geita Gold FC ilipoteza mchezo huo Jumapili (Machi 06) katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, baada ya kuuhamisha mchezo huo kutoka mkoani Geita kwenye Uwanja wa Nyankumbu.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Geita Gold FC Simon Shija amesema hawana budi kuwapongeza wachezaji wao kwa kazi kubwa waliyoifanya katika mchezo huo, licha ya kushindwa kuwika katika Uwanja wao wa nyumbani.

Shija amesema wachezjai wao kwa ujumla walionyesha kupambana hadi mwisho, na dhamira yao ilikua ni kuibuka na ushindi ambao ungewapa alama tatu, ila mambo yalikwenda tofauti.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii